Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unasisitiza, hadhi ya mazungumzo ya upatanishi kwa Sahara ya Magharibi hairidhishi

UM unasisitiza, hadhi ya mazungumzo ya upatanishi kwa Sahara ya Magharibi hairidhishi

Ripoti ya karibuni ya KM kuhusu Sahara ya Magharibi imekaribisha, kwa ridhaa kuu, ahadi za makundi husika na mzozo huo, yaani Serikali ya Morocco na kundi la ukombozi wa Sahara Magharibi la Frente POLISARIO, kuendelea kushiriki kwenye majadiliano ya upatanishi. Lakini KM alionya kwamba kasi ya mazungumzo haitoweza kusarifiwa bila ya kwanza \'kukwamua mzoroto uliopo wa kisiasa, kwa moyo wa kuelewana na uhalisia wa kutoka pande zote mbili.\' Ripoti ya KM ilisema hali ya mazungumzo ilivyo sasa hivi haikubaliki kamwe, katika kusukuma mbele juhudi za upatanishi na ni lazima irekibishwe.