Ofisi ya OHCHR kufungwa Angola

18 Aprili 2008

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu inatarajiwa kusitisha kazi zake nchini Angola mnamo tarehe 31 Mei, baada ya wenye madaraka katika taifa hilo kukataa kutia sahihi makubaliano ya jumla ya kuanzisha rasmi ofisi ya kulinda na kutekeleza haki za binadamu nchini humo. ~ ~

Louise Arbour, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu kufuatia taarifa hiyo alikumbusha kwamba taifa la Angola bado linakabiliwa na vizingiti aina kwa aina kwenye juhudi za kupigania haki za binadamu. Alisema "anasikitika lakini anahishimu" uamuzi wa Serikali wa kutoridhia maafikiano ya kuwepo ofisi rasmi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Angola.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter