Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei kubwa ya chakula duniani inafananishwa na gharika ya 'tsunami bubu'

Bei kubwa ya chakula duniani inafananishwa na gharika ya 'tsunami bubu'

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetahadharisha ya kuwa kupanda kwa bei ya chakula, kwa kiwango kikubwa katika siku za karibuni, ni tatizo adhimu la kihistoria ambalo Shirika halijawahi kukabiliwa nalo tangu lilipobuniwa miaka 45 iliopita. Kwa mujibu wa WFP maafa yanayotokana na bei kubwa ya chakula katika soko la kimataifa ni janga linalofanana na kile walichokiita \'tsunami bubu\', hali ambayo inahatarisha maisha ya watu milioni 100 ziada, takriban katika kila pembe ya dunia. Umma huo, kwa kulingana na fafanuzi za WFP, bado unasumbuliwa na unaendelea kuzama kwenye mazingira ya ufukara. WFP imetoa ombi maalumu kwa wahisani wa kimataifa kuchangisha dola milioni 756 zinazohitajika kuhudumia kidharura umma muhitaji wa kimataifa. Hivi sasa WFP imeshapokea nusu tu ya jumla hiyo.