Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchukuaji wa sensa mpya waanzishwa rasmi Sudan

Uchukuaji wa sensa mpya waanzishwa rasmi Sudan

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani Sudan Kusini (UNMIS) limeipongeza Serekali ya Sudan, na pia kundi la SPLM, kwa utiaji sahihi Maafikiano ya Amani ya Jumla (CPA) katika 2005, kitendo ambacho kimewezesha tukio la kihistoria kutekelezwa nchini kuanzia Aprili 22, ambapo shughuli muhimu za kuhesabu raia wa Sudan katika nchi nzima zilianzishwa rasmi, kwa madhumuni ya kuandaa matayarisho ya uchaguzi wa taifa utaofanyika mwakani.