Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dereva mwengine wa WFP auawa Darfur

Dereva mwengine wa WFP auawa Darfur

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kwamba mnamo Aprili 21, Mohammed Makki El Rasheed dereva alioajiriwa na UM alipigwa risasi na kuuawa barabarani wakati alipokuwa anapeleka shehena ya chakula Darfur kwa umma unaotegemea posho hiyo kunusuru maisha. Ajali hii ilizuka baada ya lori la Mohammed Makki kuharibika, kwenye eneo liliopo kilomita 40 kutoka mji wa Nyala, katika barabara iliopo baina ya Darfur Kaskazini na Kusini.

Marehemu Mohammed Makki amewacha watoto mayatima sita.