Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano Mogadishu kuchochea uhamaji mpya wa dharura

Mapigano Mogadishu kuchochea uhamaji mpya wa dharura

Ron Redmond, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) aliwaambia waandishi habari kwamba mapigano yaliozuka wiki hii katika mji mkuu wa Mogadishu, Usomali yamechochea tena uhamaji mpya wa raia. Watu 7,000 wanakadiriwa kulikimbia vurugu hilo wiki hii na kufululizia kwenye vitongoji viliopo karibu na Mogadishu. Uhamaji huu umeithirisha matatizo katika juhudi za kuhudumia kihali umma ambao unakadiriwa kufikia milioni moja. Idadi hii hutegemea kufadhiliwa misaada ya kihali na wahisani wa kimataifa na hadhi yao ni ile inayojulikana kama wahamiaji wa ndani ya nchi (IDPs) waliong\'olewa makwao na kukosa mastakimu ya kudumu.