Skip to main content

Waathiriwa wa mapigano Sudan walazimika kupatiwa misaada ya kihali

Waathiriwa wa mapigano Sudan walazimika kupatiwa misaada ya kihali

Naibu Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu kwa Sudan, Ameerah Haq Ijumatatu aliwaambia waandishi habari mjini Khartoum ya kuwa raia wa Darfur Magharibi, walionaswa kwenye mazingira ya mapigano yalioselelea kwenye maeneo yao kwa sasa wanahitajia kupelekewa misaada ya kihali, haraka iwezekanavyo, ili kunusuru maisha. Bi Haq alitoa ombi hili la hadhara linaloyataka yale makundi yanayopambana kieneo kuwaruhusu wafanyakazi wanaohudumia misaada ya kiutu kuendeleza shughuli zao bila ya pingamizi wala vikwazo, na kuwawezesha kuwapelekea raia muhitaji posho la kunusuru maisha.