Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Eneo la vurugu katika JKK limeongezewa wanajeshi na MONUC

Eneo la vurugu katika JKK limeongezewa wanajeshi na MONUC

Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (MONUC) limelaani kwa kuzuka tena karibuni vurugu maututi kwenye jimbo la Ba-Kongo. MONUC imeripoti kuwa imewajibika kupeleka wanajeshi zaidi kwenye eneo la mtafaruku na kujaribu kuzuia vurugu lisienee au kutapakaa zaidi. Kadhalika, Mkuu wa MONUC na Mumbne Maalumu wa KM, Alan Doss alitoa mwito maalumu uyatakayo makundi yote yanayohasimiana kuwacha mapigano haraka. Kwa mujibu wa MONUC watu saba waliuawa kutokana na tukio hilo la mapigano na darzeni ya watu walijeruhiwa.~