Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Bodi la Utawala la Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi wa Kimataifa (ILO) leo limeanza kikao chache cha 301, ambapo miongoni mwa masuala yatakayozingatiwa itajumuisha utekelezaji wa haki za kimsingi za ajira katika baadhi ya nchi, ushirikiano kati ya sekta za binafsi na kiraia, pamoja na kusailia shughuli za ILO za kuwasaidia wafanyakazi wahamiaji na udhibiti ubaguzi dhidi yao. ~

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limehadharisha kuzuka kwa maradhi ya kuvu (fungus) wenye kuharibu mazao ya ngano katika Iran. Inakhofiwa pindi tatizo hili halitodhibitiwa mapema kuna hatari ya maradhi haya kusambaa katika mataifa ya Asia ya Kusini na Kati – hususan yale mataifa yanayozalisha ngano kwa wingi, mathalan, Afghanistan, India na Pakistan. Maradhi haya ya kuvu huenezwa kwa upepo na yana uwezo wa kugharikisha mashamba ya ngano kwa mkumbo mmoja. Kuvu haribifu waligunduliwa zamani katika mataifa ya Afrika Mashariki na Yemen.