Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufufuaji wa utalii ni muhimu kwa uchumi Kenya, asema Mkuu wa UNEP

Ufufuaji wa utalii ni muhimu kwa uchumi Kenya, asema Mkuu wa UNEP

Achim Steiner, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) kabla ya kuondoka Nairobi Alkhamisi kuelekea Berlin, Ujerumani kunapofanyika maonyesho makubwa ya utalii duniani, aliwaambia wanahabari kwamba huduma za uchumi, pamoja na udhibiti bora wa viumbe anuwai, zinaweza kusawazishwa kwa natija za taifa zima, pindi utalii wa asili utafufuliwa tena nchini Kenya.

Vipi hali ya nchi hivi sasa? Tulimuuliza suala hilo Askofu Margareth Wanjiro, Mbunge wa Jimbo la Uchaguzi la Starehe katika Nairobi, ambaye yupo hapa Makao Makuu akihudhuria kikao cha mwaka cha Kamisheni ya UM juu ya Haki za Wanawake, yaani Kamisheni ya CSW.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.