Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia ya walimu Sudan kufadhiliwa na Ujapani misaada ya kuimarisha taaluma

Mamia ya walimu Sudan kufadhiliwa na Ujapani misaada ya kuimarisha taaluma

Serikali ya Ujapani imelifadhilia Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) msaada wa dola milioni 8.7 zitakazotumiwa mnamo miaka mitatu ijayo, kuwapatia mafunzo ya ualimu, Sudan kusini, mamia ya watu wanaohitajika kusomesha watoto wa eneo hilo.

Mashirika ya UM juu ya wahamiaji (UNHCR), maendeleo ya watoto (UNICEF) pamoja na yale yanayohusika na huduma za chakula na lishe bora (WFP) na (FAO) yatajumuika kuisaidia Wizara ya Elimu Sudan Kusini kufikia lengo lake la kuhitimisha walimu 10,000 katika 2011.