Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa misaada maridhawa unazorotisha huduma za amani ulimwenguni

Ukosefu wa misaada maridhawa unazorotisha huduma za amani ulimwenguni

Jean Marie Guehenno, Naibu KM Msaidizi juu ya Operesheni za Ulinzi wa Amani Duniani na Mkuu wa Idara ya DPKO, mapema wiki hii aliiambia Kamati Maalumu ya Baraza Kuu Inayosimamia Huduma za Amani za UM kwamba tunakabiliwa na tatizo sugu la kuendeleza yale mafanikio yaliopatikana karibuni ya kurudisha utulivu na amani katika maeneo kadha yenye migogoro, kwa sababu ya kupungua kwa shauku ya jamii ya kimataifa kujua kinachoendelea kwenye mazingira kama hayo, na vile vile kuporomoka sana kwa michango ya kimataifa na misaada inayohitajika kuendeleza shughuli za amani.