Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaongeza kasi kurudisha wahamiaji Sudan Kusini

UNHCR yaongeza kasi kurudisha wahamiaji Sudan Kusini

Kuanzia mwezi Machi Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kuongezeka kwa idadi ya wahamiaji wa Sudan Kusini wanaorejeshwa makwao, kila wiki, kutoka mataifa jirani. Mwanzo wa 2008 wahamiaji waliokuwa wakisaidiwa kurejea Sudan kusini kwa khiyari ilikuwa 600 kwa wiki na sasa hivi idadi hiyo imepindukia 3,000 kwa wiki, hali ambayo inatazamiwa kuendelea katika miezi ijayo.~