Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya Sahara ya Magharibi yaendelea kwenye Jimbo la New York

Mazungumzo ya Sahara ya Magharibi yaendelea kwenye Jimbo la New York

Ijumapili ya jana, tarehe 16 Machi, katika wilaya ya Manhasset, Long Island iliopo kwenye vitongoji vya Jiji la New York kulianzishwa duru ya nne ya yale mazungumzo kuhusu suala la Sahara ya Magharibi, mazungumzo ambayo yalihudhuriwa na wawakilishi wa makundi yote husika na mgogoro huo, yaani Morocco na kundi la Frente POLISARIO na yanaongozwa na Mjumbe Binafsi wa KM, Peter van Walsum.