Mitambo ya simu kutoka ITU inahudumia waathiriwa wa mafuriko Zambia

18 Machi 2008

Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Mawasiliano ya Kimataifa (ITU) limepeleka Zambia mitambo 25 inayobebeka ya satalaiti, kwa ajili ya kutumiwa kufufua tena shughuli za viunganishi vya mawasiliano ya simu, huduma ambazo ziliharibiwa sana na mafuriko makali yaliopiga karibuni taifa hilo.

Mitambo hii inayobebeka ya satalaiti, na yenye uwezo wa kuhamishwa kidharura, imeshasaidia kuongoza kwa sasa operesheni za Serikali ya Zambia na zile za mashirika yanayohudumia misaada ya kiutu katika kufarijia kihali ule umma ulioathirika vibaya na mafuriko.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud