Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya Sahara Magharibi yamekhitimisha duru ya nne mjini New York

Mazungumzo ya Sahara Magharibi yamekhitimisha duru ya nne mjini New York

Duru ya nne ya mazungumzo ya siku mbili kuzingatia suala la Sahara ya Magharibi imemaliza mijadala yake Ijumanne katika wilaya ya Manhasset, kwenye jimbo la New York. Vikao viliongozwa na Mjumbe wa KM kwa Sahara ya Magharibi, Peter van Walsum, na kuhudhuriwa na wawakilishi wa Morocco, Chama cha Ukombozi cha Frente Polisario pamoja na wajumbe kutoka mataifa jirani ya Algeria na Mauritania.

Van Walsum kwenye taarifa ya pamoja, aliyoitoa baada ya mazungumzo, alisema wajumbe husika walilenga mazungumzo yao zaidi kuhusu taratibu za kuyatekeleza maazimio 1754 na 1783 ya Baraza la Usalama, ambayo yote yaliyahimiza makundi husika kujadiliana haraka, bila ya masharti ya mwanzo, na kwa kuaminiana kwa minajili ya kufikia suluhu ya kisiasa inayoridhisha, ya kudumu na ya haki.