Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dokezo ya ripoti ya OHCHR juu ya vurugu Kenya baada ya uchaguzi

Dokezo ya ripoti ya OHCHR juu ya vurugu Kenya baada ya uchaguzi

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Binadamu (OHCHR) Ijumatano imetoa ripoti yenye kuelezea matokeo ya ziara ya wiki tatu Kenya, iliofanywa na wataalamu mwezi uliopita ambapo walichunguza kiini halisi cha machafuko na vurugu liliolivaa taifa hilo kufuatia uchaguzi wa Raisi katika Disemba 27, 2007.~

Ripoti ya Ofisi ya Kamishna Mkuu juu ya Haki za Binadamu (OHCHR) ilikuwa ni ya kurasa 20 na ilisisitza kwamba licha ya kuwa uchaguzi wa Raisi ulikiuka baadhi ya taratibu za kawaida, hali ambayo ripoti inaamini ilikuwa ndio chanzo kilichochea vurugu, hata hivyo kuna sababu fulani fulani nyenginezo za msingi ambazo pia zilipalilia vurugu na machafuko nchini – mathalan, matatizo ya ubaguzi, suala la kunyimwa haki ya kupiga kura na shida ya umasikini na hali duni.

Tutakupatieni taarifa kamili kuhusu ripoti ya Ofisi ya Kamisheni Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu kuhusu Kenya katika siku za mbele.