Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la kudhibiti ugaidi duniani lazingatiwa tena na BU

Suala la kudhibiti ugaidi duniani lazingatiwa tena na BU

Ijumatano Baraza la Usalama (BU) lilikutana kwenye kikao cha hadhara kuzingatia kazi za ile Kamati ya Kukabiliana na Ugaidi Duniani. Mkurugenzi Mkuu wa Kamati hiyo, Mike Smith alibainisha kwenye taarifa yake kupatikana maendeleo makubwa ya kimataifa kwenye zile juhudi za kukabiliana na vitendo vya kigaidi; na alithibitisha nchi nyingi zimefanikiwa kuingiza kwenye sheria zao za kitaifa kanuni zenye kutambua kihakika kuwa kosa la ugaidi ni jinai ya kuadhibiwa kisheria.

Baada ya kikao hicho Baraza la Usalama lilipitisha, kwa kauli moja, azimio la kuongeza muda Kurugenzi Kuu ya Kamati ya Kukabiliana na Ugaidi mpaka mwisho wa 2010. Kurugenzi hii imedhaminiwa madaraka ya kufuatilia namna mataifa yanavyotekeleza mapendekezo ya kupambana na janga la ugaidi katika dunia.