Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUC yaripoti hali tulivu Katanga Kaskazini kwa wahamiaji kurejea

MONUC yaripoti hali tulivu Katanga Kaskazini kwa wahamiaji kurejea

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika JKK (MONUC) limeripoti kwamba hali hivi sasa katika jimbo la Katanga Kaskazini ni shwari, na mazingira ya utulivu yamesharejea na wahamiaji 20,000 wa Kongo waliopo uhamishoni Tanzania na Zambia wanaweza kurejea makwao kuanzisha maisha.