Skip to main content

Usomali imetimiza tukio la kihistoria kufyeka polio nchini

Usomali imetimiza tukio la kihistoria kufyeka polio nchini

Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitisha wiki hii ya kuwa walimwengu wamejipatia ushindi mkuu, na wa kutia moyo, kwenye zile huduma za afya ya jamii kwa kudhibiti maradhi ya kupooza/polio katika Usomali.

Kwa mujibu wa ripoti ya WHO taifa la Usomali lilifanikiwa kukomesha maradhi ya polio kwenye maeneo yake baada ya kubainika ya kuwa hakujasajiliwa hata mtu mmoja aliyeambukizwa na virusi vya ugonjwa huo, katika nchi nzima, kwenye kipindi cha mwaka mmoja. Mapema wiki hii, mwandishi habari wa Redio ya UM, Derrick Mbatha alifanya mahojiano, kwa njia ya simu, na Afisa wa WHO anayehusika na idara ya udhibiti wa polio duniani, Oliver Rosenbauer, aliopo Geneva. Rosenbauer alielezea taratibu zilizotumiwa Usomali na jamii ya kimataifa kudhibiti bora ugonjwa wa polio.

Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaa ya mtandao.