Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yajiandaa kusaidia kihali Comoros pindi yatahitajika

Mashirika ya UM yajiandaa kusaidia kihali Comoros pindi yatahitajika

Mashirika ya UM yanayohusika na misaada ya kiutu - ikijumuisha zile taasisi zinazohusika na maendeleo ya watoto, UNICEF; afya, WHO; Misaada ya Dharura, OCHA na pia usalama, UNDSS – yametangaza kipamoja kwamba yameshijiandaa kuhudumia misaada ya dharura Masiwa ya Comoros, pindi msaada huo utahitajika baada ya kuripotiwa kwamba vikosi vya Serikali, vikisaidiwa na majeshi ya Umoja wa Afrika kutokea Sudan na Tanzania walishambulia kisiwa cha Anzuwani Ijumanne, na kumwondosha raisi muasi Mohamed Bacar.

Imetangazwa na wenye masdaraka Comoros kwamba wataidhinisha kuundwa serikali mpya ya muda katika Anzuwani mnamo mwisho wa wiki, serikali ambayo itashika madaraka mpaka uchaguzi mpya utakapofanyika kisiwani huko katika siku zijazo.