Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa Tanzania anasailia ajenda ya mwaka ya KMJ

Mjumbe wa Tanzania anasailia ajenda ya mwaka ya KMJ

Wawakilishi wanachama wa Kamisheni juu ya Maendeleo ya Jamii (KMJ) walikusanyika karibuni kwenye Makao Makuu ya UM mjini New York kuhudhuria kikao cha mwaka, ili kuzingatia masuala anuwai yanayohusu huduma za kuimarisha maendeleo ya jamii mathalan, taratibu za kufuatwa kimataifa kukuza ajira, nidhamu ya kukimu mahitaji ya umma unaozeeka pamoja na kuzingatia yale masuala yenye kutatanisha maisha ya watu walemavu duniani.~

Ernest Ndimbo, Mkurugenzi wa Ajira kwenye Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Watoto Tanzania anaelezea maoni ya taifa lake kuhusu ajenda za kikao cha mwaka cha Kamisheni ya UM juu ya Maendeleo ya Jamii, na pia anasailia taratibu za kuchukuliwa na mataifa yanayoendelea kutekeleza mapendekezo ya mkutano, wakati wanakabiliwa na mfumo wa utandawazi ambao baadhi ya Mataifa Wanachama hudai unawakaba kiuchumi na kimaendeleo.

Sikiliza idhaa ya mtandao kwa taarifa kamili.