Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo ya karibuni Burundi kuisumbua Kamisheni ya Ujenzi wa Amani

Maendeleo ya karibuni Burundi kuisumbua Kamisheni ya Ujenzi wa Amani

Kamisheni ya UM Kufuatilia Ujenzi wa Amani kwenye yale mataifa yaliobuka kutoka mazingira ya vurugu na mapigano, imewasilisha ripoti mpya kuhusu hali nchini Burundi ambapo ilisema jumuiya ya kimataifa ina wasiwasi juu ya uamuzi wa lile kundi la Palipehetu-FNL wa kujitoa na kutoshiriki kwenye Utaratibu wa Jumla wa Pamoja wa Kusimamia na Kuthibitisha Kusitishwa kwa Mapigano, mradi ambao ulianzishwa 2006.

Kadhalika, ripoti imeinasihi Serikali ya Burundi kujitahidi kufanya kila iwezalo kusuluhisha tofauti ilizonazo na viongozi wa Palipehetu-FNL. Wakati huo huo Baraza la Usalama lilitakiwa lifuatilie, kwa uangavu mkubwa zaidi, juhudi zote za kurudisha amani katika Burundi.