Skip to main content

UNHCR imefanikiwa kurejesha Sudan Kusini wahamiaji 100,000

UNHCR imefanikiwa kurejesha Sudan Kusini wahamiaji 100,000

Wiki hii Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti tukio la kihistoria ambapo operesheni za kurejesha wahamiaji wa Sudan wa Kusini zilirajisiwa kukamilisha jumla ya wahamiaji 100,000 waliofanikiwa kurejeshwa makwao, kwa khiyari, kutoka mataifa jirani ya Uganda, Kenya na Ethiopia. Wahamiaji hawa walikuwa wakiishi kwa muda mrefu kwenye nchi jirani kufuatia mapigano yaliozuka kwenye maeneo yao katika siku za nyuma.

Operesheni za kuwarudisha wahamiaji Sudan Kusini zilianzishwa rasmi na UNHCR mwaka 2005, na zilikusudiwa kuwasaidia wahamiaji kuanzisha maisha mapya baada ya utulivu na amani kushika mizizi nchini mwao. Fungu kubwa la wahamiaji hawo walitaka kurejea makwao kabla ya majira ya mvua kuanza mwezi Mei, na baadhi yao walisema walitaka kuwahi kuandikishwa kwenye sensa ya taifa itakayofanyika nchini mwezi Aprili (05-30) mwaka huu.