Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali katika Kenya

Hali katika Kenya

Alkhamisi KM Ban Ki-moon alihutubia kikao cha ufunguzi cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia. Kwenye risala yake alitoa mwito maalumu wenye kuwataka viongozi wa Afrika kuhimiza viongozi wenziwao, na vile vile umma wa Kenya, kushirikiana kurudisha kipamoja utulivu nchini mwao, na aliwataka wajariibu kusuluhisha tofauti zao kwa mazungumzo na majadiliano, na kutekeleza taratibu za kidemokrasia.

Ijumaa KM Ban alizuru Kenya na alipokuwepo Nairobi, alisisitiza tena hisia zake mbele ya waandishi habari ambapo alibainisha “kusikitishwa pakubwa kuhusu kiwango cha mapigano na ugomvi uliojiri nchini kati ya raia. Hali hii, aliongeza kusema, ndio iliyozusha mateso, watu kungo’lewa makwao, vifo vingi kutukia, visivyostahamilika, na kuongeza uharibifu uliovuka mipaka.” KM alisisitiza tena kwamba hali hii haikubaliki, na ni lazima ikomeshwe, halan.

Kupata fafanuzi ziada juu ya hali, kwa ujumla, nchini Kenya, tulifanya mahojiano ya simu na Mhariri wa NTV-Kenya, Shaban Ulaya.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.