Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wahudumia Misaada ya Kiutu na Kisiasa Kenya

UM wahudumia Misaada ya Kiutu na Kisiasa Kenya

Tumekuandalieni ripoti mbili zinazoelezea operesheni za mashirika ya UM yanayohusika na huduma za dharura za wahamiaji (UNHCR) na pia operesheni za kugawa miradi ya chakula duniani (WFP) kwa waathiriwa wa maafa.

Kadhalika, tuna taarifa inayosailia huduma za Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) za kugawa chakula, kwa umma ulioathiriwa zaidi na machafuko ya karibuni Kenya. Taarifa za WFP zinasema shirika limefufua tena operesheni zake katika baadhi ya majimbo, baada ya utulivu kuonekana kurejea kieneo.

WFP imethibitisha jumla ya wahamiaji wa ndani ya nchi waliong’olewa maskani Kenya, kwa sasa, na ambao watahitajia kufadhiliwa misaada ya kiutu kutoka wahisani wa kimataifa imefikia watu 300,000 ziada.

Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaa ya mtandao.