Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu Duniani (UNIFEM) imeihimiza jamii ya kimataifa kuongeza juhudi za kukomesha kihakika, tabia hatari ya kutahiri watoto wa kike. UNIFEM imependekeza kwa nchi wanachama kuheshimu haki za wanawake pamoja na watoto wakike pote duniani, mwito ambao ulitangazwa Februari 7 (08) katika kipindi ambacho walimwengu walikuwa wakiiadhimisha na kuiheshimu Siku ya Kimataifa dhidi ya Ukeketaji wa Wanawake.

KM Ban Ki-moon ameliambia Baraza Kuu la UM kwamba walimwengu wanalazimika kushikrikiana kidharura, ili kujikinga na hatari ya mifumko ya migogoro ambayo anaashiria itachochewa na upungufu wa maji safi duniani.

WFP imeanzisha kampeni mpya yenye mada isemayo “Jaza Kombe” kwa makusudio ya kuchangisha fedha, na pia kuamsha hisia za jamii ya kimataifa ili kusaidia kukomesha tatizo la njaa kwa mamilioni ya wale watoto wa skuli katika mataifa yanayoendelea ambao desturi hutegemea posho la chakula kutoka UM; kampeni ambayo imeshirikisha mchezaji maarufu wa mpira wa futboli wa kutoka Brazil, Kaka, pamoja na Raisi wa Ghana ambaye pia ni Raisi wa Umoja wa Afrika, John Agyekum Kufuor na vile vile Meya wa mji wa Milan, Utaliana, Letizia Moratti.

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF) limeripoti kutoridhia maamuzi ya kamisheni ya kijeshi ya Marekani iliopo Guantanamo Bay, iliokusudia kumshtaki Omar Khadr (raia wa Kanada) kama ni mtu mzima aliyeshiriki kwenye jinai ya vita, licha ya kuwa alipokamtawa nchini Afghanistan mwaka 2002, mtoto huyu alikuwa na umri wa miaka 15, umri ambao UNICEF inaamini kisheria hauwezi kutumiwa kushtaki, kwa kulingana na vigezo vya kanuni za kimataifa juu ya haki za watoto, kwa sababu wakati Omar alipokamatwa alikuwa chini ya umri wa kushtakiwa kama mtu mzima wa miaka 18.