WFP kuongeza misaada ya kiutu kwa wakimbizi wa Usomali katika Yemen
Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza kuwa litapanua operseheni za kuhudumia chakula wahamiaji 43,000 wa Usomali waliopo Yemen sasa hivi. Wahamiaji hawa walihajiri makwao kukimbia mapigano. WFP imetoa mwito maalumu uitakayo wahisani wa kimataifa kufadhilia dola milioni 4 zinazohitajika kuhudumia kidharura operesheni zake kwa umma husika, huduma ambazo zinatarajiwa kuendelezwa mpaka Januari 2010.