Vifo vya saratani vinaendelea kuangamiza umma, vyatakiwa kudhibitiwa kimataifa: WHO

8 Februari 2008

Ripoti mpya iliyowasilishwa na Dktr Margaret Chang, Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la Afya Duniani (WHO) ilihadharisha kwamba licha ya kuwa kasi imezidi kimataifa kwenye juhudi za kudhibiti matumizi ya tumbaku, bado anaamini huduma hizi ni haba na haziridhishi. Alisisitiza ya kuwa kunahitajika msukumo ziada wa kadhia hiyo katika Mataifa yote Wanachama.~

Tarehe 04 Februari imewekwa kando na UM kuwa ni Siku ya Kukumbushana juu ya Janga la Saratani Duniani.

Sikiliza kwenye idhaa ya mtandao uchambuzi wa mtaalamu wa WHO kuhusu tatizo la saratani na tumbaku.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter