Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waathiriwa wa mafuriko kusini ya Afrika wanahitajia dola milioni 89 kukidhi mahitaji ya kiutu

Waathiriwa wa mafuriko kusini ya Afrika wanahitajia dola milioni 89 kukidhi mahitaji ya kiutu

Hivi karibuni Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imetoa mwito maalumu wa kufadhiliwa mchango wa dola miloni 89 na wahisani wa kimataifa kwa makusudio ya kuisaidia Serikali za Malawi, Msumbiji, Zambia na Zimbabwe kukabiliana na athari za mafuriko yaliolivaa eneo lao hivi karibuni. Imeripotiwa mafuriko yaliangamiza maelfu ya nyumba na kuharibu mavuno, na vile vile kusababisha watu nusu milioni kufiliska na kutegemea misaada ya dharura ya kimataifa kunusuru maisha. Kadhalika inatazamia kutumia mchango huo kuyasaidia mataifa husika kujiandaa kidharura pindi mvua zitanyesha tena kwa wingi na kusababisha mafuriko haribifu mengine ambayo huenda yakaathiri watu 805,000.