Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMEE yahamisha, kwa muda, wafanyakazi na vifaa kutoka Eritrea

UNMEE yahamisha, kwa muda, wafanyakazi na vifaa kutoka Eritrea

Mnamo wiki hii Shirika la UM linalohudumia ulinzi wa amani mipakanai Ethiopia/Eritrea limeanzisha uhamisho wa muda wa wafanyakazi na vifaa kutoka Eritrea na kuelekea maeneo yaliopo ndani ya Ethiopia.

Balozi Ricardo Alberta Arias wa Panama, Raisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Februari, alisema kwenye taarifa yake kwamba Mataifa 15 Wanachama wa Baraza hilo wanashtumu, kwa kauli moja, uamuzi ya Serikali ya Eritrea kutoshirikiana na UM katika kusuluhisha mvutano wao, hasa ilivyokuwa Eritrea inaendelea kuweka vikwazo aiana kwa aina dhidi ya misafara ya UM inayoelekea Ethiopia hivu sasa. Kadhalika, UM umearifiwa kwamba hautoweza tena kupokea nishati wala vifaa vyengine vya kuhudumia mahitaji ya watumishi wake na pia kukidhi mahitaji ya operesheni za ulinzi wa amani mipakani kutoka ile kampuni kampuni ya Eritrea ilioitiana sahihi mkataba maalumu wa kuipatia UNMEE huduma hizo. Kwa mujibu wa KM hii ni hali ya kutia wasiwasi kwa sababu UNMEE imebakiza akiba haba ya posho la dharura la kuhudmia shughuli zake.

Kwa hivyo, KM Ban amewataka wenye madaraka Eritrea kukomesha, haraka, vizingiti vyao dhidi ya uhamisho wa muda wa UNMEE wa kupeleka Ethiopia vifaa na wafanyakazi. Alinansihi Eritrea kutekeleza majukumu ya kushirikiana na UM kama ilivyoafikiana pale ilipotia sahihi na kuidhinisha mikataba ya kimataifa juu ya suala hili.