Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango wa UM kuhudumia misaada ya kiutu na amani Kenya

Mchango wa UM kuhudumia misaada ya kiutu na amani Kenya

Imeripotiwa kwamba Waziri wa Habari wa Kenya Samuel Poghiso alitangaza karibuni kuwa kumeandaliwa tume maalumu ya uchunguzi itakayotumiwa kupeleleza kama baadhi ya watu na makundi fulani nchini yalitumia vyombo vya mawasiliano ya redio kuchochea chuki za kikabila kufuataia matokeo ya uchaguzi, kitendo ambacho kinavunja sheria za taifa. ~

Idara ya Habari ya UM majuzi ilifanya mahojiano na Francis Deng, Mshauri Maalumu wa KM juu ya Masuala Yanayohusu Mauaji ya Halaiki ambaye alisailia lile tatizo linaoambatana na utumiaji wa baadhi ya vyombo vya habari nchini Kenya kuchochea chuki za kikabila.

Sikiliza jawabu ya Deng pamoja na fafanuzi za Naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro kuhusu suala hili.