Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lazungumzia hifadhi ya watoto wanaonaswa kwenye mazingira ya mapigano

Baraza la Usalama lazungumzia hifadhi ya watoto wanaonaswa kwenye mazingira ya mapigano

Baraza la Usalama liliitisha kikao maalumu cha siku moja katika Makao Makuu, ambapo wajumbe kadha wa kadha walishauriana hatua za kuchukuliwa na Mataifa Wanachama ili kuwalinda watoto wenye umri mdogo dhidi ya vitimbi vya udhalilishaji, mateso na uonevu wanaokabiliwa nawo wakati wanapozongwa na mazingira ya migogoro na mapigano, unyanyasaji ambao umeonekana kukithiri katika miaka ya karibuni, hasa kwenye yale maeneo yalioghumiwa na kukumbwa na hali ya mapigano.~

Bi Radhika COOMARASWAMY, Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Masuala ya Hifadhi ya Watoto kwenye Mazingira ya Mapigano alipohutubia kikao alikumbusha ya kuwa wakati umewadia wa kutekeleza, kwa vitendo, zile ahadi za vikao vilivyopita za kuwapatia watoto wadogo, pote duniani, ulinzi imara wa kisheria dhidi ya mateso ya wale watu wenye kukiuka, kwa makusudi, haki za mtoto wakati mapigano yanapozuka kwenye maeneo yao.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.