Juhudi za kutumia nishati mbadala Tanzania kupunguza umasikini

15 Februari 2008

Katika ziara niliyofanya Tanzania siku za nyuma, nilibahatika kuhudhuria warsha maalumu wa siku mbili katika Mkoa wa Kigoma, ambapo kulisailiwa taratibu za kukuza haraka maendeleo ya uchumi kwa kutumia nishati mbadala vijijini. Miongoni mwa mambo yaliyotatanisha wanawarsha ni kwamba utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hususan ile inayoambatana na matumizi ya nishati, huwa haulingani na ratiba ya mradi.

Bariki Kaale, Mtaalamu aliyetayarisha warsha huo, kutoka ofisi ya UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) aliiambia Idhaa ya Redio ya UM kwamba ni muhimu kushirikiana na wananchi kuhakikisha wanapata nishati endelevu na pia rahisi kwa ajili ya maendeleo ya sekta zote zinazoambatana na ile miradi ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa yetu ya mtandao.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter