Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Edward Luck, raia wa Marekani ameteuliwa kuwa Mshauri Maalumu wa KM wa UM juu ya masuala yanayohusu hifadhi-kinga na misaada ya kiutu ya dharura penye uhasama wa kitaifa.

Mataifa ya Costa Rica, Iceland, New Zealand na Norway pamoja na miji minne, ikijumuika na makampuni makuu ya kimataifa matano yametia sahihi mradi mpya wa UM wa kuanzisha mtandao utakaotumiwa kuharakisha mataifa kukomesha uharibifu wa mazingira unaotokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Alkhamisi Februari 21 iliadhimishwa kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Kuheshimu Lugha ya Mama. Kadhalika katika siku hiyo hiyo Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lilianzisha rasmi harakati za Mwaka wa Kimataifa Kuhifadhi Lugha za Kimataifa. Kwa mujibu wa ripoti za UNESCO nusu ya lugha, karibu elfu saba, zinazotumiwa ulimwenguni sasa hivi huwa zinakabiliwa na hatari ya kuangamia na kupotea, na inakadiriwa, takriban katika kila wiki mbili lugha moja ya kimataifa huangamia na kutoweka milele katika dunia.