Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

'Fujo na ghasia za makundi ni mutlaki' kuonya Mjumbe wa UM Liberia

'Fujo na ghasia za makundi ni mutlaki' kuonya Mjumbe wa UM Liberia

Ellen Margrethe Loj, Mjumbe Maalumu wa UM katika Liberia alipokutana Alkhamisi na raia waliohudhuria mkutano wa hadhara katika mji wa Tappita, wilaya ya Nimba nchini Liberia, alitoa nasaha kali iliyowaonya kujiepusha na tabia karaha ya makundi kutumia nguvu na fujo na kuchuka haki mikononi mwao.Alisema tabia hii inatengua sheria za kitaifa na kimataifa.

Onyo la Mjumbe wa UM lilitolewa baada ya shambulio la karibuni ambapo kundi kubwa la watu walioanzisha fujo walichoma moto steshini mpya ya polisi kwenye mji wa Tappita, baada ya kugundua mwanamke mmoja wa miaka 38 aliuawa kwa uzembe. Vurugu hilo liliwalazimisha wanajeshi wa Bangladesh, wa Shirika la UM la Ulinzi Amani Liberia (UNMIL)kuwahamisha kidharura wale watuhumiwa wa makosa ya kuua waliokuwa kizuizini kwenye steshini iliyounguzwa moto.