Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Masuala ya Mgogoro na waasi wa LRA Uganda Kaskazini, Joaquin Chissano, Raisi wa zamani wa Msumbiji, amenakiliwa kuripoti kupatikana maafikiano ya kutia moyo mwisho wa wiki, baada ya Serikali ya Uganda na waasi wa LRA walipotiliana sahihi kwenye mji wa Juba, Sudan Kusini, mwafaka wa kudumisha kuacha kupigana.~

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF) likijumuika na jumuiya ya kufadhilia watu masikini ruzuku, linalojulikana kama Matunzo ya Dubai kwa Madhaifu (Dubai Cares) yametangaza kuwa yatashirikiana kipamoja kuendeleza huduma za ilimu katika Djibouti, na kulenga zaidi kwenye huduma za kuwavua watoto wa kike na tatizo la kutojua kusoma na kuandika, fungu ambalo mara nyingi hunyimwa nafasi za kuelimishwa.

Ijumatatu, Naibu KM Asha-Rose Migiro aliwaambia wakurugenzi wa vyeo vya juu, pamoja na viongozi wa biashara waliohudhuria kikao maalumu cha Baraza la UM juu ya Maendeleo ya Uchumi na Jamii (ECOSOC) kuwa wakiamua kukithirisha michango yao ya fedha kusaidia nchi zinazoendelea kiuchumi itayahamasisha mataifa hayo kuufyeka umasikini na hali duni kwa haraka, na kuyawezesha kukamilisha, kwa wakati, yale Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti matokeo ya utafiti ulioabshiria kwamba walimwengu watabarikiwa mbolea maridhawa ya kukifu mahitaji yote ya uzalishaji chakula na nishati kutoka viumbe hai mnamo miaka mitano ijayo.