Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imesafirisha Kenya misaada ziada ya kiutu

UNHCR imesafirisha Kenya misaada ziada ya kiutu

Mnamo mwisho wa wiki iliopita, Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) lilipeleka nchini Kenya mahema 2,345 yatakayotumiwa na makumi elfu ya zile familia zilizong’olewa makwao baada ya machafuko kufumka nchini mwanzo wa mwaka kufuatia uchaguzi.

Mahema haya yalisafirishwa kwa ndege ya aina ya Boeing 747-400 ambayo iliyapakia kutoka ghala za vifaa vya dharura vya UM ziliopo Dubai. Mahema mengine 2,655 yanatazamiwa kupelekwa kwa meli na yanatarajiwa kuwasili Mombasa katika siku za karibuni. Kwa mujibu wa UNHCR makumi elfu ya raia waliongo’lewa makwao (IDPs) nchini Kenya bado wanaishi kwenye mastakimu ya muda kwenye vituo 200 ziada viliotawanyika katika sehemeu mbalimbali za nchi.