Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yajitolea kufufua elimu ya msingi Liberia

UNICEF yajitolea kufufua elimu ya msingi Liberia

Ann Veneman, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF), ambaye anazuru Liberia wiki hii, ametangaza kufadhilia taifa hilo msaada wa dola milioni 20 zitakazotumiwa kufufua tena sekta ya ilmu ya msingi, ambayo iliharibiwa na vile vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoshtadi nchini humo kwa muda wa miaka kumi na tano.

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa ni thuluthi moja tu ya wanafunzi wa skuli za praimari Liberia wanaojaaliwa fursa ya kumaliza darasa la tano. Liberia ni moja ya mataifa machache duniani ambapo fungu kubwa la vizazi vilivyotangulia hujua kusoma na kuandika kushinda vizazi vya sasa.