Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za kupunguza umaskini Tanzania kwa kutumia nishati mbadala (Sehemu ya Pili)

Juhudi za kupunguza umaskini Tanzania kwa kutumia nishati mbadala (Sehemu ya Pili)

Katika makala iliopita, tulikupatieni sehemu ya kwanza ya mazungumzo na Bariki Kaale, mtaalamu wa nishati katika ofisi ya Dar es Salaam ya Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Miradi ya Maendeleo Duniani (UNDP). Alisaiilia juhudi za wanavijiji kutumia kile alichokiita “nishati endelevu” iliyo rahisi, ambayo umma wa kawaida wataimudu na itawasaidia kukuza maendeleo yao kwa ujumla.

Moja katika mipango iliyoanzishwa ya kuwasaidia wanavijiji kuyatekeleza hayo ilikuwa ni katika matumizi ya majiko sanifu. Mtaalamu wa nishati wa UNDP anaelezea natija za kutumia majiko sanifu kwa wanavijiji Tanzania.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao