Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahajiri wa Burundi kufadhiliwa makazi na UNHCR

Wahajiri wa Burundi kufadhiliwa makazi na UNHCR

Katika miaka mitano iliopita Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limefadhilia makazi wahamiaji 58,000 waliorejea Burundi kutoka matifa jirani na nchi za kigeni, msaada ambao uliowawezesha kujenga nyumba mpya na kupata matumaini ya maisha bora kwa siku zijazo.

UNHCR inaashiria mahitaji ya msaada huu kutoka wahamiaji wa Burundi waliopo nje itakithiri katika 2008. Msaada huu hufadhiliwa zaidi familia na aila za WaBurundi zinazoongozwa na wanawake na watu wakongwe.