Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jimbo la Wasomali wa Ethiopia lakabiliwa na tatizo la njaa

Jimbo la Wasomali wa Ethiopia lakabiliwa na tatizo la njaa

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imearifu ya kuwa hali katika lile eneo la Ethiopia la Ogaedn ambapo huishi raia wenye asili ya Kisomali, linaitia wasiwasi jamii ya kimataifa kwa sababu ya kutanda kwa tatizo la chakula.

Tatizo hili lilisababishwa na mvua haba, pamoja na kuadimika kwa eneo la malisho ya wanyama, upungufu wa maji na vikwazo vya bidhaa kutoka mataifa jirani. Hivi sasa Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP)limeanzisha operesheni za kugawa tani 17,000 za chakula kwa raia muhitaji wa eneo husika.