Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utekelezaji wa MDGs Kijijini Mbola, Tanzania - Kilimo na Mazingira (Sehemu ya Kwanza)

Utekelezaji wa MDGs Kijijini Mbola, Tanzania - Kilimo na Mazingira (Sehemu ya Kwanza)

Mnamo siku za nyuma tulianzisha vipindi maalumu kuhusu juhudi za kizalendo za wenyeji wa kijiji cha Mbola, katika Mkoa wa Tabora, Tanzania za kuharakisha utekelezaji wa ile miradi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) ili kuikamilisha kwa wakati, kama ilivyopendekezwa na maafikiano ya jumuiya ya kimataifa katika mwaka 2000. Miradi hii ipo chini ya uongozi wa UM na hufadhiliwa na wahisani mbalimbali wa kutoka sehemu kadha wa kadha duniani.

Katika makala zilizopita tulizingatia namna sekta za afya na jamii kwenye Kijiji cha Mbola zinavyohudumiwa na wanavijiji, ikiwa miongoni mwa harakati za kuufyeka umasikini na hali duni kwenye eneo lao. Ripoti ya awali leo hii, itazingatia namna Malengo ya MDGs yanavyohudumiwa katika sekta za kilimo na mazingira. Nilipozuru Kijiji cha Mbola nilipata fursa ya kuzungumza na Eliezer N. Kagya, Kaimu Naibu wa Kilimo na Mazingira ambaye alitufafanulia namna shughuli zao zinavyoendelezwa katika juhudi za kupunguza umasikini kieneo.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.