Wapatanishi wa UM/UA watangaza matumaini mema kurudisha amani Darfur

Wapatanishi wa UM/UA watangaza matumaini mema kurudisha amani Darfur

Wajumbe Maalumu wa Kimataifa kwa Darfur, yaani Jan Eliasson akiwakilisha Umoja wa Mataifa (UM), pamoja na Salim Ahmed Salim anayewakilisha Umoja wa Afrika (UA), baada ya kuzuru Sudan kwa wiki moja, ambapo walikutana kwa mashauriano na wawakilishi wa Serikali pamoja na wajumbe wa makundi ya waasi, waliripoti kuwa na matumaini ya kutia moyo kwamba wataweza kufufua tena karibuni yale mazungumzo ya Sirte ya kukomesha mzozo wa jimbo la vurugu la Sudan magharibi.

Kwa jawabu kamili, na vile vile fafanuzi ziada juu ya hali kijumla katika Darfur, sikiliza idhaa ya mtandao.