Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sauti za wanakijiji zasailia Mradi wa Milenia Mbola

Sauti za wanakijiji zasailia Mradi wa Milenia Mbola

Katika makala zilizopita tulieleza kwamba Mbola ilikuwa ni moja ya vijiji vya Milenia viliopo Afrika kusini mwa Sahara, vilivyochaguliwa na UM kufanywa vijiji vya mfano, ambavyo uzoefu wake ulitarajiwa kutumiwa kuongoza udhibiti bora wa miradi ya MDGs katika sehemu nyengine za taifa, na pia katika Afrika, kwa ujumla. Tangu Miradi ya Milenia ilipoanzishwa hadi leo huduma kadha wa kadha ziliekezwa Kijijini Mbola, Tanzania, hususan katika sekta za kilimo, elimu, miundo mbinu, afya na kadhalika, shughuli ambazo zilionekana kushika mizizi ya kutia moyo katika kukabiliana na matatizo ya umasikini, na katika huduma za kuwapatia wanakijiji wa Mbola natija za kuwanyanyua kimaisha.

Makala yetu, kwa leo, itawakilisha sauti za wataalamu wahusika, pamoja na wanakijiji, ambao tulipata fursa ya kuzungumza nawo pale mtayarishaji vipindi alipozuru Chuo cha Utafiti cha Tumbi, Kijijini Mbola, ambapo alikutana na wanafunzi waliokuwa wakifundishwa taratibu za uekezaji katika viwanda vya kushindika chakula.

Sikiliza kipindi kamili na sauti za wanakijiji kwenye idhaa ya mtandao.