Skip to main content

Mpatanishi wa UA kwa Darfur ana matumaini ya kutia moyo juu ya amani

Mpatanishi wa UA kwa Darfur ana matumaini ya kutia moyo juu ya amani

Wajumbe wa UM na UA wanaoshughulikia suala la Darfur, yaani Jan Eliasson na Salim Ahmed Salim, karibuni walikamilisha duru nyengine ya zile juhudi za kufufua tena mazungumzo ya jumla kuhusu amani katika Darfur, baina ya Serikali ya Sudan na makundi ya waasi. Jumbe Omari Jumbe, Ofisa wa Habari wa Shirika la Ulinzi wa Amani la UM Sudan (UNMIS) alipata fursa ya kumhoji Mpatanishi wa Umoja wa Afrika Salim hivi majuzi alipozuru mji wa Juba, Sudan kusini.