Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo na Tabibu wa Hospitali ya Muhimbili, Tanzania kuhusu udhibiti bora wa UKIMWI

Mazungumzo na Tabibu wa Hospitali ya Muhimbili, Tanzania kuhusu udhibiti bora wa UKIMWI

Takwimu mpya za Taasisi ya UNAIDS na Shirika la Afya Duniani (WHO)zimethibitisha kwamba katika kipindi cha sasa karibu watu wazima milioni 33.2 na watoto milioni 2.7 chini ya umri wa miaka 15 wanaishi na virusi vya UKIMWI (VVU). Lakini, kwa bahati mbaya watu wanaoishi na VVU mara nyingi hutengwa na kufedheheshwa na jamii zao kwa sababu ugonjwa huo huambatanishwa na tabia na vitendo visivyolingana na tamaduni za kijadi. Kwa hivyo umma huu hujikuta wanabaguliwa na kunyimwa haki zao za kimsingi.

Mkutano wa DPI/NGOs uliambatana na 'Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani'. Muktadha wa maadhimisho ya mwaka huu ulitilia mkazo umuhimu wa kuwa na uongozi bora kwenye harakati zote za kimataifa za kukabiliana na matatizo yanayozushwa na UKIMWI duniani. Miongoni mwa viongozi walioshiriki kwenye mkutano uliofanyika Makao Makuu alikuwemo Dktr Jessie Mbwambo wa Taasisi ya Magonjwa ya Akili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, iliopo Dar es Salaam, Tanazania. Nilichukua fursa ya kufanya mahojiano na Dktr Mbwambo ambaye alituelezea namna taifa lake linavyojishirikisha kwenye huduma za kuwapatia wagonjwa husika tiba na uangalizi ufaao dhidi ya UKIMWI.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.