Skip to main content

Aliyetoa ushahidi bandia mbele ya Mahakama ya ICTR kuhukumiwa kifungo cha miezi tisa

Aliyetoa ushahidi bandia mbele ya Mahakama ya ICTR kuhukumiwa kifungo cha miezi tisa

Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) imemhukumu kifungo cha miezi tisa jela yule shahidi aliyetambuliwa kwa alama ya jina la GAA, ambaye alituhumiwa kutoa ushahidi usio sahihi mble ya mahakama baada ya kula kiapo.

Kitendo hiki kilitafsiriwa kudharau mamlaka ya mahakama. Ripoti za UM zinasema Shahidi GAA alikiri kosa lake la kuinyima Mahakama ya ICTR, kwa makusudi, fursa ya kutekeleza haki.