MONUC yawataka wapiganaji waasi kusalimisha silaha

7 Disemba 2007

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (MONUC) limetoa mwito uliowahimiza wapiganaji waasi kusitisha mapigano na kusalimisha silaha, na kuchukua fursa hiyo ya baadaye kujiunganisha na mpango wa kitaifa utakaowachanganyisha, kwa utartaibu ulio halali, na maisha ya kawaida ya jamii nchini.

Mwito huu ulitolewa baada ya kufumka mapigano katika mwanzo wa mwezi Disemba, kati ya Vikosi vya Serikali na wafuasi wa Jenerali Mtoro, Laurent Nkunda katika sehemu ya Mushake, iliopo kilomita 40 kaskazini-magharibi ya Goma katika jimbo la mashariki ya JKK. Vikosi vya taifa hivi sasa vinasaidiwa kihali na majeshi ya ulinzi wa amani ya UM ya MONUC, mchamngo ambao unalingana na madaraka waliodhaminiwa na maazimio kadha ya Baraza la Usalama kuhusu huduma za amani nchini.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter