Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unaadhimisha Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani - Disemba Mosi

UM unaadhimisha Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani - Disemba Mosi

Mwaka huu ‘Siku ya Kupambana na Ukimwi Duniani’- ambayo hukumbukwa kimataifa kila mwaka mnamo Disemba mosi - ilitimiza miaka 20 tangu jumuiya ya kimataifa ilipoanza kuiheshimu siku hiyo katika 1988. Mamilioni ya watu duniani huiadhimisha Siku ya Kupiga Vita UKIMWI kwa nia mbalimbali.

Tangu 1988 pale Shirika la Afya Duniani (WHO) lilipopendekeza kwa umma wa Mataifa Wanachama kujiunga kipamoja kupiga vita UKIMWI, ugonjwa huu umezagaa na kuwa miongoni mwa matatizo sugu hatari yanayofungamana na maisha ya karne ya ishirini na moja. Janga la UKIMWI limesambaa na kuenea takriban katika kila pembe ya ulimwengu wetu – na limechukua umbo la kijinsia ambapo imeripotiwa fungu kubwa la waathiriwa wa maradhi haya huwa ni wanawake, bayana iliothibitishwa na takwimu za UM zenye kuonyesha nusu ya watu waliopatwa na kuishi na VVU duniani hivi sasa ni wanawake!

Dktr Jessie Mbwambo, wa Taasisi ya Magonjwa ya Akili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, mjini Dar es Salaaam, Tanzania alizuru Makao Makuu ya UM wiki iliopita, na alifanya mazungumzo na Idhaa ya Redio ya UM. Dktr Mbwambo alizungumzia uhusiano wa ziara yake na juhudi za kimataifa katika kukabiliana na tatizo la UKIMWI. Kadhalika, alitoa nasaha maalumu kuambatana na Siku ya Kupiga Vita UKIMWI Duniani na kuhimiza umma katika maeneo ya Afrika Mashariki kutopwelewa, na kuwa waangavu, kwenye juhudi za kukabiliana na janga hili.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.